RUANGWA LIWALE KILWA NACHINGWEA LINDI RURAL LINDI URBAN  

LINDI RURAL

1.0 UTANGULIZI:

 

Halmashauri ya Wilaya ya Lindi ni moja kati ya Halmashauri sita za Mkoa wa Lindi.

Halmashauri hii ilianzishwa tena kama halmashauri ya wilaya chini ya Sheria ya Mamlaka ya Serikali za mitaa - “The Local Government Act” (District Authorities) namba 8 ya mwaka 1982 baada ya kufutwa kwa Serikali za Mitaa mwaka 1972 kutokana na Sheria ya Madaraka Mikoani.

Lengo likiwa ni kusogeza huduma za jamii karibu zaidi na wananchi.


1.1 MAHALI ILIPO
Halmashauri ya Wilaya ya Lindi ipo kati ya latitudo 90.31’ na 100.45’ kusini mwa mstari wa Ikweta na kati ya longitudo 380.4’ na 40o Mashariki ya Greenwich. Upande wa Kaskazini inapakana na Wilaya ya Kilwa, Mashariki inapakana na Bahari ya Hindi, Kusini inapakana na mkoa wa Mtwara, kwa upande wa Magharibi inapakana na Wilaya ya Ruangwa.

1.2 ENEO LA WILAYA

Halmashauri ya Wilaya ina ukubwa wa eneo la Kilometa za mraba 7,538. Kati ya hizo eneo la nchi kavu ni Kilomita za mraba 6,355 na eneo la maji ni Kilomita za mraba 1,183. Eneo linalofaa kwa kilimo ni jumla ya Kilomita za mraba 5,718 na eneo linalotumika kwa kilimo kwa mwaka ni kilomita za mraba 1,009 sawa na asilimia 17.6 ya eneo linalofaa kulimwa.

1.3 UTAWALA:

Kiutawala wilaya ya Lindi imegawanyika katika majimbo mawili ya uchaguzi ambayo ni Mchinga na Mtama. Kutokana na sensa ya idadi ya watu na makazi ya mwaka 2002. Wilaya hii inayo Tarafa 10, Kata 28, vijiji 125 na vitongoji 807.

1.4 IDADI YA WATU:

Kutokana na sensa ya watu na makazi ya mwaka 2002, halmashauri ya wilaya ya Lindi ilikuwa na watu wapatao 214,882. Kati ya hao, 102,112 (47.5%) ni wanaume na 112,770 (52.5%) ni wanawake. Maoteo (projection) ya idadi ya watu kwa mwaka 2007 yanaonyesha wilaya hii ina watu wapatao 221,328. Msongamano wa watu ni 29 kwa kila kilometa moja ya mraba ya nchi kavu. Ongezeko la watu kwa mwaka ni asilimia 0.6 %.

1.5 HALI YA HEWA:

Hali ya hewa ni ya joto kwa wastani ambayo hufikia nyuzi joto 27o (centrigrade) na hupungua hadi nyuzi joto 24o (centigrade) wakati wa baridi. Sehemu za mwinuko za Rondo ndio zenye baridi zaidi kuliko sehemu za Pwani. Halmashauri ya wilaya ya Lindi ina msimu mmoja tu wa mvua ambao huanza mwanzo wa mwezi Novemba na kumalizika mwezi Aprili kila mwaka. Kiwango cha mvua kwa mwaka ni milimita 1,000.

1.6 SHUGHULI ZA KIUCHUMI

Shughuli kuu ya kiuchumi katika Wilaya ni kilimo. Shughuli zingine zinazofaywa na wananchi ni uvuvi, ufugaji nyuki na Biashara ndogondogo.Mazao ya chakula ni pamoja na mahindi, mtama, Mpunga na muhogo. Mazao ya biashara ni Korosho, Ufuta na Nazi.

1.6.1 Hali ya umaskini:

Halmashauri ya Wilaya ya Lindi ni moja kati ya halmashauri zenye wakazi maskini zaidi hapa Tanzania. Wastani wa pato la mkazi wa Halmashauri ya Wilaya kwa mwaka ni Tshs.270,000/= kiasi ambacho ni chini ya kiwango cha Kitaifa cha Tshs.277,870/=.

Hali ya umaskini inajionyesha kutokana na viashiria (indicators) vya kuwa na asilimia kubwa ya vifo vya watoto, vifo vya akinamama wajawazito na kutojua kusoma na kuandika. Kati ya sababu zinazobainishwa kuwa na kiwango hiki cha umaskini ni utegemezi wa vifaa duni katika uzalishaji mali (kwa mfano matumizi ya jembe la mkono na zana duni za uvuvi).

1.6.2 Mikakati wa kupunguza umaskini wa pato:

Halmashauri ya Wilaya imejiwekea mikakati mbalimbali ya kuinua hali ya uchum,i kupunguza na kuondoa tatizo la njaa kwa kuwataka wananchi kulima angalau ekari 2 za mazao ya chakula kwa kila kaya kati ya kaya 44,000 zinazojishughulisha na kilimo. Pia kulima angalau ekari 2 za mazao ya biashara ikiwa ni pamoja na kupanua kilimo cha mazao mchanganyiko. Kaya hizo 44,000 zote zikilimwa ekari 2 za mazao ya chakula jumla ya ekari 88,000 zitakuwa zimelimwa na uzalishaji utakuwa ni tani 61,600. Mahitaji ni tani 58,824. Hivyo kutakuwa na ziada ya tani 2,776.


1.7.0 HALI YA WATUMISHI:
Halmashauri ya Wilaya ya Lindi ina jumla ya watumishi 1333 ikiwa ni watumishi wanawake 415 na wanaume 918.

1.7.1 UPUNGUFU WA WATUMISHI:
Halmashauri ya Wilaya ya Lindi ina upungufu mkubwa wa watumishi. Upungufu huu unatokana na sababu kuu mbili;-

- Dhana iliyojengeka miongoni mwa Watanzania kuwa kusini hakufai kuishi. Hii husababisha watumishi wanaopangwa kuja kufanyakazi kusita kuripoti. Hata hivyo kusini sasa kumefunguka baada ya kukamilisha barabara ya Kibiti – Lindi – Mingoyo.
- Upungufu wa Wataalam wenyeji hivyo huzilazimu Taasisi na Halmashauri kutafuta wataalam nje ya Lindi hata kwa kada za chini.

Idara zilizoathirika sana na upungufu ni pamoja na Elimu (237),Maendeleo ya Jamii(26), Kilimo/Mifugo (47), Maliasili (72), Fedha (13) na Afya (300). Mwaka 2006/2007 Wizara ya Afya ilitupangia watumishi thelathini na sita (36) lakini ni watumishi watumishi (5) tu walioripoti hadi sasa. Aidha Wahasibu sita tulipangiwa na OWM – TAMISEMI ameripoti mmoja tu.


1.7.4 TAARIFA ZA WAKUU WA IDARA NA VITENGO 2007/2008:
Halmashauri ya Wilaya ya Lindi ina Idara kumi (10).
(1) Utawala na Utumishi
(2) Fedha
(3) Mipango na Biashara
(4) Ardhi, Maliasili na Mazingira
(5) Ujenzi
(6) Maji
(7) Afya
(8) Elimu
(9) Kilimo/Mifugo na Ushirika
(10) Maendeleo ya Jamii

Uteuzi wa Wakuu wa Idara unazingatia muundo uliotajwa hapo juu. Hadi Octaba, 2008 ni Wakuu wa Idara saba (7) ndiyo walio na barua rasmi za uteuzi toka mamlaka mbalimbali za ajira. Wakuu wa Idara tatu (3) wanakaimu nafasi zao, ambazo ni Idara za Maji, Maliasili na Afya.

Aidha, Halmashauri inavyo vitengo viwili (2) ambavyo ni Ukaguzi wa Ndani na Sheria na Usalama.


1.8.1 ELIMU

1. Elimu ya Awali

Elimu ya awali hutolewa kwa watoto wenye umri kati ya miaka 5 hadi 6 ambao kwa wakati huo huwa wanajiandaa kuanza darasa la kwanza. Zipo shule za awali 96 zenye jumla ya wanafunzi 4,035. Kati yao, wavulana ni 2,042 na wasichana 1,993 Kati ya shule hizo, hakuna shula za watu binafsi au mashirika na zote 95 ni za serikali. Mahitaji halisi ya shule hizo ni 123 kwa mwak 2008. Shule zilizopo ni 90% ya mahitaji halisi. Kuna upungufu wa shule 27.

Katika shule hizi za awali kuna madarasa 86 tu na hivyo kuwa na upungufu wa madarasa 37. Mkakati uliopo ni kuhakikisha kuwa kila shule ya msingi inafungua darasa la awali lenye majengo ya kudumu na samani za kutosha kwa kushirikisha nguvu za wananchi.


5. MEMKWA: (Mpango wa Elimu ya Msingi kwa walioikosa)

Wilaya ina madarasa ya Memkwa 104 na vituo 7 vyenye mchanganuo ufuatao.
- Kundi rika la kwanza 3,574 wakiwemo Wav. 1,906,Was 1668 madarasa 76 ya kundi rika la kwanza.
- Kundi rika la pili Wav 1,372 na Was 1,441 Jumla 2813 yakiwemo madarasa 28 yenye vituo 7. Jumla kuu 6,387 madarasa 104 vituo 7.

1.8.2 HUDUMA ZA AFYA:

1. Takwimu za Afya:

Kuna hospitali 1, vituo vya afya 5 na zahanati 38 kama inavyoonekana katika jedwali hapa chini:

Jedwali Na 3: Huduma za Afya zilizopo

Kituo cha huduma

Mmiliki

Idadi ya vitanda

Serikali Taasisi Binafsi Jumla Serikali Taasisi
Hospitali

0

1 0 1 1 254
Kituo cha afya

4

1 0 5 56 0
Zahanati

36

2 0 38 6 0

Kwa upande wa Hospitali bado inahitajika moja zaidi kwani kisera Hospitali moja inatakiwa ihudumie watu 100,000. Kutokana na idadi ya watu waliopo kunahitajika hospitali moja zaidi, na kwa kukamilisha hilo kituo kimoja cha afya kinapanuliwa kuwa hospitali. Upungufu wa madaktari bado ni tatizo kwani kitaifa Daktari mmoja anatakiwa ahudumie wagonjwa 25,000 (1:25,000). Hali halisi katika Halmashauri ya Wilaya ya Lindi ni Daktari mmoja anahudumia wagonjwa 107,441 (1:107,441).


2.0 HUDUMA ZA UCHUMI:

2.1 UJENZI – BARABARA:

Halmashauri ya Wilaya ya Lindi ina jumla ya barabara zenye urefu wa km.621 katika mchanganuo ufuatao:-

Jedwali Na 6: Mchanganuo wa urefu wa barabara wilayani.

Na. Aina ya barabara Urefu / Idadi Lami Udongo / Changarawe
Changarawe Udongo
1 Barabara kuu Km 198 103 95 -
2 Barabara za mkoa Km 78   22 56
3 Barabara za wilaya Km 308   40 268
4 Barabara za vijiji Km 37 - - 37
5 Madaraja ya zege 5      
6 Karavati / drifti 36      
CHANZO: Idara ya ujenzi 2008

2.2 MAWASILIANO NA UCHUKUZI:

- Halmashauri ina huduma za mawasiliano na uchukuzi kama ifuatavyo
- Viwanja vya ndege 1
- Mitandao simu za mikononi (Vodacom, Celtel, Tigo, Zantel – (4)
- Huduma za posta 1
- Huduma za Benki NMB,NBC,CRDB, na Benki ya posta - (4)
- Radio calls - 1
- Barua pepe - 1
- Fax - 4

2.3 KILIMO:

1. Mazao ya chakula.
Mazao ya chakula yaliyolimwa ni mahindi, mtama, mpunga, mbaazi, muhogo na kunde.2.5 ARDHI, MALIASILI NA HIFADHI YA MAZINGIRA


1. ARDHI.
- Mipaka yote ya Vijiji 125 katika Halmashauri ya Wilaya ya Lindi imepimwa na ramani yake ipo.
- Jumla ya Vijiji 10 ambavyo ni Mkwajuni, Likong’o, Likwaya, Madingo, Muungano, Mandwanga, Njonjo, Mtegu, Namunda na Nandambi vimewezeshwa kutengeneza mpango wa matumizi bora ya ardhi. Hii ni sawa na asilimia 100 ya lengo lililowekwa.
- Uundaji wa mabaraza ya ardhi.
- Mabaraza ya Ardhi ya Kata 28 yameundwa sawa na asilimia 100 ya utekelezaji.
- Mabaraza ya Ardhi ya Vijiji 125 yameundwa sawa na asilimia 100 ya utekelezaji mwaka 2007/2008
- Viwanja vilivyopimwa ni 39, ambavyo ni asilimia 39% ya lengo la kupima viwanja 100. Mashamba yaliyopimwa ni 2 kati ya 20 ambayo ni asilimia 20% ya lengo tuliyojiwekea.

2.8 UTALII
Halmashauri ya Wilaya ya Lindi imekwisha ainisha vivutio mbalimbali vya utalii na juhudi zinafanywa za kuvitangaza ili kuvutia wawekezaji.
Vivutio hivyo ni pamoja na: -

- Kuwepo kwa fukwe nzuri za kuvutia – Vijiji vya Sudi, Shuka, Mmumbu, Kikwetu, Mbanja, Mchinga na Kijiweni;
- Kuwepo kwa viwanja (Beach plots) ambavyo vinaweza kutumika kwa kujenga hoteli za kitalii vijiji vya Sudi, Shuka, Mmumbu, Kikwetu, Mbanja, Mchinga na Kijiweni;
- Kuwepo kwa aina mbalimbali za samaki ikiwa ni pamoja na kuonekana kwa samaki aina ya kisukuku (Coelocanth) ambaye alipotea mamilioni ya miaka iliyopita katika bahari ya Hindi;
- Kuwepo kwa misitu yenye utajiri wa bioanuwai na mabonde mazuri ya kuvutia katika Tarafa za Rondo, Nyangamara, Mipingo, Mtama, Nangaru, Mingoyo, Sudi, Mchinga, Ng’apa na Milola;
- Eneo la Tandaguru katika Tarafa ya Mipingo yalikuwa makazi ya mijusi wakubwa sana (Dinosaurs) ambao waliishi na kupotea duniani mamia ya mamilioni ya miaka iliyopita.
- Mila na desturi za wakazi pia ni kivutio cha utalii (cultural tourism), kwa mfano Jando na Unyago.


 
   
INVESTMENTS OPPORTUNITY
Forest
Mining
Fishing
Industry
   
TOURISM
Wildlife
Tourist Hotel
Kilwa
 

Copyright 2007 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi,
P.O.BOX 1054,Lindi , Simu Na:
023-2202098, FAX: 023-220-2502